Back to top

BIDEN:MIMI NDIYE MTEULE, HAKUNA WA KUNIONDOA.

04 July 2024
Share

Rais wa Marekani Joe Biden, ameweka wazi kuwa bado ataendelea kusalia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Novemba mwaka huu, huku akisisitiza kuwa yeye ndiye mteule wa Chama cha Democratic, na hakuna mtu wa kumuondoa wala haondoki. 

Joe Biden alifanya kazi ya kuwatuliza wanachama wa Democrats na wafanyakazi wakuu, kwenye kampeni yake siku ya Jumatano, kwani ripoti zilidokeza kwamba alikuwa akiangazia mustakabali wake, baada ya mdahalo wake mbaya na mpinzani wake Donald Trump wiki iliyopita.

Awali Rais Biden, alikula chakula cha mchana kwa faragha na Makamu wa Rais Kamala Harris, katika Ikulu ya White House, huku uvumi ukiibuka kuwa huenda angechukua nafasi ya Biden kama mgombea wa chama katika uchaguzi wa Novemba.