Back to top

BIL. 37.7 KUSAIDIA KUTOKOMEZA MALARIA NCHINI

09 April 2024
Share

Wadau wa mfuko wa Afya wamechangia kiasi cha Shilingi Bilioni 37.7/=, kupitia ufadhili wa moja kwa moja wa Kituo cha Afya (DHFF), (2021-2025), ili kusaidia kutokomeza malaria nchini ifikapo mwaka 2030.
.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu, wakati akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Mhe. Didier Chassot, ambao ni moja ya wadau hao, katika ofisi za Wizara hiyo, zilizopo Jijini Dodoma, ambapo amemshukuru kwa msaada huo na ahadi ambazo zimetolewa na Uswisi katika kusaidia Sekta ya Afya kupitia michango mbalimbali ya ruzuku.
.
Amesema, lengo la jumla la mradi ni kuchangia kutokomeza Malaria ifikapo mwaka 2030 kupitia ushirikishwaji wa wadau wa Kitaifa, kisekta na kikanda kwa kushawishi mijadala ya sera za Kimataifa na miongozo ya kiufundi.
.
Aidha, Waziri Ummy ameiomba Serikali ya Uswizi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kutokomeza magonjwa ya ngono ikiwa ni pamoja na VVU, mimba zisizotarajiwa, ndoa za utotoni, ukatili wa kijinsia pamoja na kusaidia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii (CHWs) ambao wana jukumu katika kutoa huduma muhimu za Afya kwa Jamii.