Back to top

BOT KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI

25 February 2025
Share

Benki Kuu ya Tanzania (BOT)imesema inatambua mchango wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kama kiunganishi muhimu kati ya taasisi hiyo na jamii katika kuelimisha kuhusu masuala ya uchumi na fedha.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa tawi la Benki Kuu Mtwara, Ndugu Nassoro Omary, akimuwakilisha Naibu Gavana wa Benki hiyo Bw.Julian Banzi Raphael katika ufunguzi wa semina ya waandishi wa habari inayofanyika Mkoani Mtwara .

Semina hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa juhudi za Bot katika kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uelewa wa kina kuhusu majukumu ya Bot na mchango wake kwenye uchumi.

Kutokana na umuhimu huo mkubwa kwa vyombo vya habari ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Waandishi wa habari kuendelea kutumia nafasi zao kujenga uchumi wa nchi katika nafasi mbalimbali walizonazo.

Awali, Meneja Uhusiano wa BoT, Vicky Msina ameeleza kwamba lengo kubwa kukutana na waandishi ni kukuza uelewa wao kuhusu masuala yanayohusu benki kuu na kujenga uhusiano wa kuwezesha kuwa karibu na wananchi kupitia vyombo vyao vya habari kwa lengo la kufikisha taarifa kwa haraka.

Semina hiyo imewakutanisha waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Ruvuma na Zanzibar.