
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimelaani vikali kitendo cha kuzuiliwa kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe.Tundu Lissu, kuingia nchini Angola, ambako alipaswa kushiriki mkutano muhimu kuhusu masuala ya Demokrasia
Mbali na Mhe. Lissu, viongozi wengine wa upinzani kutoka Tanzania, Kenya na Uganda na nchi zingine wamezuiliwa kuingia nchini humo bila maelezo ya msingi.
Taarifa ya CHADEMA, imeeleza kuwa inafuatilia kwa karibu ili kubaini sababu za zuio hilo na kuhakikisha haki za kidemokrasia za viongozi wa upinzani zinalindwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa