Back to top

CHAN 2025, AFCON 2027 MAANDALIZI YAIVA 

30 October 2024
Share

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro,  amefanya ziara ya kukagua miundombinu ya michezo katika uwanja wa Shule kuu ya Sheria na uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Jijini  Dar es Salaam, ambavyo vitatumika kwa mazoezi wakati wa mashindano ya CHAN 2025 na AFCON 2027.

Katika ziara hiyo Mhe. Ndumbaro aliambatana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu  Tanzania (TFF) Wallace Karia, na kusema kuwa,  hadi sasa hatua iliyofikiwa inakidhi vigezo kuelekea katika mashindano hayo.

Tambua kwamba kwa mara ya kwanza Tanzania, Kenya na Uganda watakuwa wenyenyi wa mashindano hayo.