Back to top

WIZARA YA KILIMO KUWASOGEZEA HUDUMA WAKULIMA, NANENANE 2024

18 July 2024
Share

Kuelekea Maonesho ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji (NaneNane 2024), yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma kuanzia Agosti 01 - 08, 2024, Mratibu Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Wizara ya Kilimo,Bw. Zacharia Gadiye ambaye  amewakaribisha wadau mbalimbali kwenye maonesho hayo, ili kujionea namna wizara hiyo ilivyojipanga kuhakikisha wakulima na wadau wengine wa Kilimo wanapata taarifa sahihi na majibu kuhusu changamoto zinazowakabili kwa wakati.

Bw. Zacharia Gadiye amezungumza hayo, alipokutana na Waandishi wa habari katika ofisi za Wizara ya Kilimo jijini Dodoma ambapo amesema kituo hicho cha huduma kwa wateja kimeanzishwa kwa lengo la kupokea changamoto, hoja na maoni kutoka kwa wakulima na wadau wengine wa sekta ya kilimo.

Kwa upande mwingine, Mratibu huyo wa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Wizara ya Kilimo ameeleza kuwa pamoja na uwepo wa wataalamu wa ugani katika ngazi za vijiji na kata, Wizara ya kilimo imefanya juhudi za kuhakikisha kunakua na mawasiliano rahisi zaidi kati ya mkulima na wataalamu wa ugani kwa kuanzisha Kituo hicho cha Huduma kwa Wateja (Call Center).