Back to top

CRDB YAANZA KUKABILIANA NA UHABA WA MADAWATI, RUNGWE

05 July 2024
Share

Katika kuhakikisha miundo mbinu ya kujifunzia kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na sekondari inakuwa rafiki nakuleta matokeo chanya, Benki ya CRDB, imetoa madawati 50 kwa shule ya msingi mwankenja iliyopo, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya, ambayo inatajwa kuwa na uhaba mkubwa wa madawati. 
 
Akizungumza na ITV Meneja wa CRDB, Tawi la Rungwe, Bi. Devota Kalinga, amesema benki hiyo hutenga 1% ya faida yake baada ya kodi kwa ajili ya kusaidia miradi ya kijamii katika Sekta ya Elimu, Afya na Mazingira, hivyo uamuzi huo umelenga kuboresha sekta ya elimu kwa kuwapunguzia adha wanafunzi wa shule hiyo na zoezi hilo ni endelevu.
 
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Bw. Jaffar Haniu, aliyepokea madawati hayo licha ya kuipongeza benki hiyo kwa uamuzi huo ameomba igeukie na maboresho ya Shule Kongwe, wilayani humo ambazo miundombinu yake imechakaa.