Back to top

Daraja lasombwa na maji ya mvua wilayani Korogwe.

03 May 2018
Share


Wakazi zaidi ya 6,000 waliopo katika vijiji mbali mbali vilivyopo kata ya Mswaha darajani wilayani Korogwe,wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa daraja linalounganisha vijiji sita kwenda makao makuu ya kata ya Mswaha kufuatia daraja wanalotegemea kusombwa na maji ya mvua na kusababisha baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule za sekondari na msingi kushindwa kwenda shule na Ngalawa kuhofia usalama wao.

Wakizungumza na ITV katika eneo la Majengo ambalo daraja hilo limesombwa na maji ya mvua,walimu pamoja na wazazi waliokutwa wakijiandaa kuvushwa kwenye ngalawa wamesema hali ya usalama wa maisha yao ipo hatarini kwa sababu baadhi ya watu wamepoteza maisha baada ya kuanguka kwenye chombo wanachosafiria .

Kwa upande wao viongozi wa serikali ya Mswaha majengo wamesema daraja liliosombwa na maji sio tu kamba linaasaidia wananchi kuvuka kwenda kufanya shughuli za maendeleo na ni zile za kiuchumi ambazo baadhi yake zimesimama bali hata serikali inakusanya kodi katika mashamba ya mkonge yaliyopo ng'ambo ya daraja hilo .