Back to top

Dkt.Ndumbaro agiza kusimamishwa kazi mkuu wa idara ya utumishi Ilala.

02 February 2019
Share

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi Dkt.Laurean Ndumbaro amemwagiza Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam kumsimamisha kazi na kumchukulia hatua za kisheria Mkuu wa Idara ya Utumishi wa manispaa hiyo Bernatha Mwaikambo.

Aidha, ameagiza maofisa utumishi wote kuhamishwa baada ya kushindwa kushughulikia mahitaji ya watumishi wa manispaa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma amesema manispaa ya Ilala ni ya kwanza nchini kwa kuwa na malalamiko mengi ya watumishi kwa sababu ofisa ameshindwa kuyashughulikia mahitaji hayo.

Ameyataja baadhi ya malalamiko ya watumishi wa manispaa kuwa kutokuwepo kwa taarifa kamili za upandishwaji vyeo pamoja na uwasilishwaji usioridhisha wa malimbikizo ya watumishi.