Back to top

ELIMU HUDUMA YA AFYA YA AKILI KUBORESHWA

06 March 2025
Share

Mwongozo wa elimu ya saikolojia kwa wagonjwa wa skizofrenia (ugonjwa wa akili unaosababisha fikira na hisia zisizo za kawaida) na ndugu zao kutambuliwa rasmi kwenye miongozo ya tiba ili kuelimisha Jamii kuhusiana na afya ya akili.
 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa hospital ya taifa ya afya ya akili, Dr. Paul S Lawala wakati wa Kikao kazi cha na wadau wa Tafiti ya KUPAA  kwaajili ya uboreshwaji wa huduma na elimu ya afya ya akili kwa wagonjwa na zao.
 
Amesema uwepo wa muongozo wa huduma za wagonjwa wa skizofrenia utasaidia kutambua wagonjwa pamoja na familia zao na kusaidia watu wanaoumwa au watakaoumwa badaye.
 
“Utafiti huu utasaidia namna gani huduma hizi za wagonjwa wa skizofrenia pamoja na familia zao zinaweza zikapata kutambuliwa rasmi kwenye miongozo ya tiba na kusadia watu ambao wanaumwa na wengine ambao pengine watakuja kuumwa,”amesema Dkt. Lawala.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya ya Akili na Mkuu wa Kitengo cha Utafiti kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe, Dkt. Innocent   Rwiza Mwombeki amesema kuwa utafiti huo utafanyika kwa Mikoa ya Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Mbeya na Dodoma kwa lengo la kusaidia kundi la wagonjwa na ndugu zao kupunguza makali ya ugonjwa wa skizofrenia nchini.
 
“Tupo katika mwaka wa kwanza wa utafiti na utafiti huu ni wa miaka mitano,  ambapo tumepokea maoni ya wadau ambao ni Wagonjwa wa skizofrenia, waganga Wakuu wa Mikoa na wilaya na ndugu wa wagonjwa hao”, ameeleza Dkt. Mwombeki
 
Dkt. Mwombeki amesema kuwa Matokeo ya utafiti yakiwa chanya watahakikisha  wanaweka miongozo imara ya ugonjwa wa skizofrenia ili kuboresha Huduma za wagonjwa hao bila kulazwa hospitali na afua hiyo inaendana na matumizi ya dawa mgonjwa akiwa nyumbani akiuguzwa na ndugu zake.
 
Baada ya miaka mitano matokeo ya utafiti wa KUPAA yatasadia Serikali  kutengeneza miongozo ya matibabu kwa wagonjwa na kuboresha Huduma za wagonjwa wa skizofrenia kwa kuishi vizuri bila kulazwa na  kutumia dawa wakiwa nyumbani