Back to top

"GRIDI YA TAIFA INA UMEME WA KUTOSHA" RAIS SAMIA.

02 August 2024
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema mfumo wa gridi ya Taifa una umeme wa kutosheleza mahitaji ya kijamii na kiuchumi.

Rais Samia ameyasema hayo wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara ya kikazi.

Rais Samia amesema, serikali inazidi kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini kupitia ujenzi na ukarabati wa miundombinu, ambapo imejenga kituo cha kupokea na kupoza umeme wilayani Kongwa, mkoani Dodoma, ambacho kitaboresha pia hali ya umeme wilayani Gairo.

Ameongeza kuwa, njia ya kusafirisha umeme kutoka kituo cha kupoza umeme cha Kongwa kwenda wilayani Gairo, imeshakamilika.