Back to top

HAKI YA MTU KUISHI IPO KIKATIBA - SAGINI

20 September 2024
Share

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Jumanne Sagini, amesema kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakuna mtu  yeyote yule anapaswa kupoteza Haki za Binadamu mwingine, ikiwa ni pamoja na kupoteza uhai. 

Sagini amesema pamoja na mambo mengine dhana ya utu na haki za kila Mwananchi lazima iheshimiwe na hivyo  kila Mwananchi ambaye anataarifa za wahalifu aripoti katika mamlaka husika 

"Nataka niwashauri Wananchi Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni alizungumza kwa hisia mambo ya mauji ya raia wasio na hatia na kinyume cha Sheria watu kujichukulia Sheria mkononi lakini matukio yanayokiuka maadili ya Taifa letu, matukio yanayohusishwa na imani za kishirikina amekemea vikali kwa kutumia Maneno Mazito." 

Aliendelea kusema "Kama wafanya uhalifu wapo miongoni mwetu kama wanajamii tunawajibu wa kuwafichua ili vyombo vya dola viwachukulie hatua.
Wakamatwe,wachunguzwe na hatimaye wakidhibitika ushahidi ukawatia hatiani wawajibishwe kwa mujibu wa Sheria."Alisema Naibu Waziri Sagini 

Aidha, Sagini amewataka Wanafunzi waliohitimu kuhakikisha wanasimamia maadili waliyoyapata walipokuwa shuleni kwa kuwa na mwenendo mwema. 

Awali, Mkurugenzi wa Shule hiyo ambaye ni Paroko wa Parokia ya Kiabakari Fr.Wojciech Adam  amesema kuwa kanisa kushirikiana na Serikali ya Poland wakiwa wadau wa maendeleo  imeendelea kutafuta wafadhili mbalimbali ili kuwekeza miundombinu ikiwemo katika sekta ya Afya na Elimu hivyo amewataka Wazazi kushiriki katika kuchangia matumizi ya kila siku ya shule ili kufanya huduma hiyo kuwa endelevu na kuondoa falsafa ya kutegemea Serikali au Wafadhili pekee.