Back to top

IFAKARA WAPONGEZWA KWA UREJESHAJI MIKOPO KWA WAKATI.

23 August 2024
Share

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Dustan Kyobya amewapongeza wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero, kwa kuwa na nidhamu na mikopo waliyochukua na kuirejesha kwa wakati.
 
Mhe. Kyobya amesema hayo wakati akifungua programu maalum ya Elimu ya Fedha kwa Umma, inayoendeshwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na washirika mbalimbali wa sekta ya fedha nchini iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo – Ifakara, Mkoani Morogoro.


 
"Najua kuwa mnachangomoto kubwa mnayoipata kupitia watoa huduma za fedha wasio waaminifu kwa kuwapa mikataba iliyoandaliwa kwa lugha ya kiingereza, wakati wengi wenu hamfahamu lugha hiyo, na kuna mtoa huduma za fedha mmoja nilishamfukuza Wilayani kwangu kwa kusumbua wananchi na mikopo yake isiyoeleweka’’ aliongeza Mhe. Kyobya.

Mhe. Kyobya aliwaagiza Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Kilosa kuhakikisha wanaratibu mafunzo ya aina hiyo yanafanyika mara kwa mara katika kata zote Wilayani Kilombero ii kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Wilaya hiyo kuhusu mikopo umiza.
 
Program maalum ya elimu ya fedha kwa maeneo ya Mkoa wa Morogoro inalenga kuwahimiza wananchi kujiwekea akiba katika Taasisi rasmi za fedha kama vile benki nk, ili kuweza kuwa na fedha kwa ajili ya shughuli za kilimo badala ya kutumia fedha zote na Kwenda kukopa mikopo umiza wakati wa kilimo.