Back to top

ITV YATWAA TUZO YA UANDISHI BORA HABARI ZA MAZINGIRA

02 August 2024
Share

Mwandishi wa habari wa ITV Mkoa wa Mbeya Rebeka Juma Kinyunyu, ameibuka mshindi wa kwanza Tuzo ya Uandishi Bora wa Habari za Mazingira mwaka 2024 upande wa runinga.

Tuzo hizo zimeandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust, ambaye Mkurugenzi wake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dr.Tulia Ackon, huku kazi 157 zikishindanishwa katika vipengele mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, amewataka wanahabari kuwa chachu ya kuandika habari za maendeleo yanayoletwa na Dr.Tulia, ambaye pia anatambua mchango wa waandishi .