Back to top

Jaffo abaini dosari ujenzi wa shule ya mfano ya serikali Dodoma.

22 June 2019
Share

Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Selemani Jaffo amekagua ujenzi wa shule ya msingi ya mfano inayojengwa na serikali jijini Dodoma huku akibaini kuwepo na dosari kwenye muundo wa majengo na kuonya yanaweza yasikidhi viwango vinavyohitajika na serikali

Shule hiyo inayojegwa katika kata ya Ipagala jijini hapa ni miongoni mwa shule tano za mfano zinazojengwa nchini ambazo vigezo vyake ni kuwa na madarasa  14 vyumba za walimu maabara ukumbi wa mikutano na jengo la utawala vyoo na miundombinu rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na viwanja vya michezo

Kutokana kubainika kwa dosari hizo mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge  amesema atakutana na uongozi wa elimu na kamati ya ujenzi ya shule hiyo ili kuangalia namna za kuzitatua kabla ujenzi huyo haujafika katika hatua kubwa
 
Kwa upande wake afisa elimu msingi halmashauri ya jiji la Dodoma mwalimu Joseph Mabelo anasema wamepokea kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 706 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na tayari mchanganuo wa matumizi umeshafanyika huku changamoto kubwa ikiwa ni upatikanaji wa vifaa vya ujenzi hasa mchanga na kokoto

Shule hizo za msingi za mfano pia zinajengwa kwenye halmashauri za Geita, Buhigwe, Masasi na Mwisenge na ni lazima ziwe kwenye maeneo yenye idadi kubwa ya watu