Back to top

Jafo aiagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa hospital uliotumia bil.1

12 July 2019
Share

Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo hajaridhishwa na ujenzi wa jengo la hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Morogoro lililotumia shilingi bilioni moja na kuagiza Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kufanya uchunguzi mara moja juu ya matumizi ya fedha hizo namna zilivyotumika. 

Akiwa Mvuha wilayani Morogoro, Waziri Jaffo amesema haiwezekani serikali itoe fedha nyingi kwa ajili ya mradi huo huku ujenzi ukishindwa kufanikishwa kwa wakati na kuhoji ni namna gani shilingi bilioni 1 zimetumika huku mradi ukiwa haujafikia hatua nzuri.

Amesema fedha zilizobaki zikiwa ni milioni 400 pekee, ambapo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo akataja sababu zilizochelewesha ingawa kila hitaji la samani za ukamilishaji likiwa tayari limenunuliwa.

Licha ya maelezo hayo Waziri Jaffo akaonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi hasa kutokana na kubaini uchache wa mafundi na kumuagiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Steven kuunda tume ya kufanya uchunguzi.