Back to top

JAJI MSTAAFU, JUXON MLAY AFARIKI DUNIA

26 May 2024
Share

Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Mhe.Juxon Isaac Mlay, amefariki dunia, wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika katika Hospitali ya Kokilaben Dhirubhai Ambani nchini India.
.
Taarifa za kifo cha Jaji huyo zimetolewa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, ambapo ameeleza kuwa Jaji Mstaafu alifariki jana Mei 25, 2024.
.
Marehemu Jaji Mlay alijiunga na Mahakama ya Tanzania Novemba 30, 2000 alipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na alistaafu Septemba 20, 2009 na kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa Mkurugenzi waMashtaka (DPP) nchini Tanzania kuanzia mwaka 1997 hadi 2000.