Back to top

Jeshi la polisi Kagera laua watu tisa wanaodhamiwa kuwa majambazi

12 October 2019
Share

Jeshi la polisi mkoa wa Kagera limewaua watu tisa wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliokutwa na silaha mbalimbali ambazo ni pamoja bomu la kutupwa kwa mkono, bunduki aina ya SMG iliyokuwa magazini yenye risasi 17, mapanga matatu na shoka moja.

Kamanda wa jeshi la polisi kamishina msaidizi Isack Msengi amesema watu wanne waliuawa kwenye eneo la tukio na watano wamefariki dunia wakati wakikimbizwa kwenye hospitali teule ya Biharamulo kwa ajili ya kupata matibabu.

Aidha, kamanda huyo pamoja na kuendelea kuwaomba wananchi waendelee kulipa ushirikiano jeshi hilo amesema majambazi waliouawa hadi sasa hawajatambuliwa japokuwa kwenye eneo la tukio baada ya askari kufanya upekuzi waliokota  
kitambulisho cha uraia kilichotolewa na nchi ya Burundi.

Mganga mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dkt.Gresmus Sebuyoya akizungumza amethibitisha kupokea  miili tisa ya marehemu hao na akasema hadi sasa bado imehifadhiwa kwenye  chumba cha kuhifadhi maiti.