Back to top

JOPO LA MADAKTARI 5 LAWASILI HOSP. YA HANDENI

09 March 2025
Share

Jopo la Madaktari Bingwa 5 kutoka Kitengo cha Mifupa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI), limewasili wilayani Handeni, mkoani Tanga, ili liweze kufanya tathmini katika kutekeleza maagizo ya Rais Mh. Dk. Samia Suluhu Hassan, alioyatoa hivi karibuni akiwa kwenye ziara wilayani humo ya kukitaka kitengo hicho kuangalia uwezekenao wa kuanzisha kitengo cha mifupa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, ambacho kitasaidia kutoa matibabu kwa watu wanao pata ajali hasa kwenye Barabara ya Segera Chalinze.

Taarifa hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Dk. Kisaka Kachua, ikiwa ni siku chache baada ya mh rais kuizindua hospitali hii ambayo kwa sasa inaonekana kuwa tegemeo kubwa kwenye ukanda huu wa barabara ya kutoka Chalinze hadi Segera eneo ambalo ajali zimekuwa zinajitokeza mara kwa mara na watu kupoteza maisha 

Taarifa hizo za ujio wa madaktari hao zinaendelea kutoa matumaini hasa kwa vijana wanaojihusisha na ubebaji wa abiria kwa kutumia pikipiki ambao wamekuwa ni wahanga wakubwa wa ajali hasa kwenye barabara hii na hapa wanaeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Bw. Saitoti Zelothe, akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, pamoja na Waheshimiwa Madiwani juu ya faida walioipata baada ya ziara ya Rais Mh. Dk. Samia Suluhu Hassan.