Back to top

KAKOLANYA AMETOROKA KAMBINI - SINGIDA FG

14 April 2024
Share

Klabu ya Singida Fountain Gate FC, imesema mchezaji wake ambaye pia ni Nahodha wa Timu hiyo, Beno Kakolanya, ametoroka kambini.
.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo imeeleza kuwa, imesikitishwa na kitendo cha mchezaji huyo, kwani ametoroka kipindi ambacho wanakabiliwa na mchezo muhimu dhidi ya Yanga na kwamba kitendo hicho kinaleta maswali mengi ukizingatia kuwa mchezaji huyo ni mzoefu na wa kutumainiwa wa timu ya Taifa.
.
Hata hivo Klabu hiyo imesema inafuatilia  taarifa zake na wachezaji wengine ambao wataonekana kuihujumu timu hiyo.