Back to top

KAPINGA: TUJITOKEZE KWA WINGI KUPIGA KURA NOVEMBA 27

26 November 2024
Share

Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM), ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Mh. Judith Kapinga, amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi Tarehe 27 Novemba 2024, kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwa pia ni utekelezaji wa haki ya kikatiba.

Mh. Judith ameyasema hayo wakati wakihitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Vijijini.

"Chama cha Mapinduzi (CCM) ni tumaini la watanzania wanaohitaji maendeleo, hivyo ifikapo Novemba 27, 2024 jitokezeni katika vituo vya kupigia kura ili mkachague Viongozi kutoka CCM watakaosimamia miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo katika Mitaa na Vijiji." Amesema Kapinga.

Ameeleza kuwa, CCM imekuwa na utaratibu mzuri wa kuwasimamia Viongozi wake ili kuhakikisha wanafikisha maendeleo kwa wananchi kama Ilani ya CCM inavyoelekeza.

Mhe. Kapinga ameweka mkazo  kuwa, miradi ya maendeleo inayopelekea  upatikanaji wa huduma za Umeme, Maji, Elimu, Afya, Kilimo na Barabara ni matokeo mazuri ya Viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya vitongoji hadi Taifa.