Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, amemtaka Mkandarasi China Railway 15 B. Group, anayejenga sehemu ya Tungamaa-Mkwaja-Mkange (Km 95.2) wilayani Pangani mkoani Tanga, kuhakikisha sehemu hiyo inakamilika ifikapo Machi mwakani.
Aidha ameagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Tanga, kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi kuongeza vifaa, wataalamu na muda wa kazi, ili kukidhi mahitaji ya mkataba.
Mhandisi Kasekenya ametoa maagizo hayo, alipokuwa akifanya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Tanga - Pangani - Saadani - Bagamoyo hadi Dar es salam, sehemu ya Tungamaa-Mkwaja-Mkange (Km 95.2).
"Barabara hii ya Dar es Salaam-Bagamoyo-Pangani-Tanga ni sehemu ya barabara ya Afrika Mashariki, inayoanzia Malindi- Lungalunga-Horohoro- Bagamoyo hadi Dar es Salaam, ikikamilika itachochea ukuaji wa uchumi wa Tanzania hususani utalii, uvuvi, biashara na huduma za uchukuzi, hivyo ni wakati wa kila mtanzania kuangalia fursa katika ukanda huu".Mhandisi Kasekenya