Back to top

KESI 25 ZA UKATILI ZAFIKISHWA MAHAKAMANI

06 December 2024
Share

 Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi  Kinondoni limefanya uzinduzi wa Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambao umebeba kauli mbiu isemayo, Kuelekea Miaka thelathini ya Beijing chagua kutokomeza Ukatili wa Kijinsia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Mtatiro Kitinkwi, amesema tayari kesi 25 za vitendo vya ukatili zimefikishwa mahakamani huku akisema kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, litaendelea kuwafikisha mahakamani na  kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ili kujenga uwelewa wa pamoja juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanywa na baadhi ya watu katika jamii.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bwana Saad Mtambule, ameiomba jamii kuendelea kutoa malezi bora kwa jamii huku akiwasihi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia huku akiitaka jamii kukemea vitendo hivyo.

Ameongeza kuwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi  katika  mapambano ya dhidi ya ukatili wa kijinsia huku akitumia fursa hiyo kulipongeza Jeshi hilo katika mapambano ya ulatili.