Back to top

KIFURUSHI CHA NAJALI, WEKEZA MBADALA WA TOTO AFYA KADI

27 May 2024
Share

Serikali imesema mfumo wa kulipia Bima za watoto kupitia Toto Afya Kadi umebadilika na sasa unafanyika kupitia utaratibu wa shule na vifurushi vya bima ya afya vya 'Najali', 'Wekeza' na 'Timiza' na kwamba wanajiunga kupitia wazazi wao.
.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Bungeni Jijini Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa, kuanza kwa utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote, utawezesha makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo watoto kupata huduma za afya kwa urahisi pasipo kuwa na vikwazo.
.
Pia, Mhe.Mollel amewataka Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa nchini kuhakikisha wanaendelea kuwapokea watoto wanaotoka katika maeneo mbalimbali na kuwapatia huduma.