Back to top

Kilele cha mbio za Uhuru 2019 zahitimishwa Ilulu mkoani Lindi.

14 October 2019
Share

Rais wa Tanzania Mhe Dkt.John Magufuli amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru kama ishara ya maadhimisho ya kilele cha mbio za Uhuru kwa mwaka 2019 katika uwanja wa Ilulu  mkoani Lindi.
  
Rais Magufuli amekabidhiwa Mwenge huo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Mzee Mkongea Ally ambaye yeye na wenzake wanaukimbiza Mwenge huo kwa siku 195 kwa mikoa yote nchini.

Awali kabla ya kukabidhiwa kwa Mwenge huo viongozi mbalimbali walitoa hotuba zake ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu amesema umekagua miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya Maji, Afya na Barabara.

Maadhimisho hayo pia ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 20 tangu baba wa taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipofariki Mjini London  Uingereza alikopelekwa kwa matibabu katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas.