Back to top

Mabula awashukia wananchi wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi.

23 June 2019
Share

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dakta.Angeline Mabula amepiga marufuku wananchi wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi kutoa pesa kwa ajili ya kugharimia usafiri wa kwenda eneo lenye mgogoro.

Akizungumza wakati wa kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ulanga, Mkoani Morogoro,Dkt.Mabula amesema, kutoa pesa ya kugharamia usafiri kwa mmoja wa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi kwenda eneo la tukio kunaweza kuleta ushawishi kwa wajumbe wake hasa kwa yule aliyetoa kiasi kikubwa cha pesa.

Dkt.Mabula amesema ni lazima wakati wa zoezi la kwenda eneo lenye mgogoro kwa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi, Mkurugenzi wa Halmashauri husika aratibu zoezi hilo huku ratiba nzima ikiwasilishwa kwa Mkuu wa Wilaya katika kipindi cha mwezi mmoja.

Aki zungumzia  uzinduzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba katika Wilaya ya Ulanga,,Dkt.Mabula amesema Serikali imezindua Baraza hilo ili  kupeleka huduma karibu na kurahisisha usikilizaji  kesi za ardhi kwa wananchi.