Back to top

Mabula azitaka halmashauri nchini kudhibiti ujenzi holela.

21 November 2019
Share

Serikali imezitaka halamashauri nchini kudhibiti ujenzi holela kwa kuhakikisha utoaji vibali vya ujenzi katika maeneo yao unazingatiwa na kusimamiwa ipasavyo.

Naibu Waziri wa Ardhi Dk.Angeline Mabula ametoa agizo hilo katika Halmashauri za wilaya za Morogoro, Mvomero pamoja na Manispaa ya Morogoro wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro.

Amesema, Halmashauri nchini zina wajibu wa kudhibiti ujenzi holela kwa kushirikiana na Watendaji wa Mitaa na kuweka taratibu ambazo hazitamruhusu mtu kufanya ujenzi wowote bila kupata kibali cha ujenzi kutoka halmashauri husika.

Dk.Mabula amesema zoezi la urasimishaji linaloendelea sasa katika maeneo mbalimbali siyo zoezi la kudumu na kulegalega kudhibiti ujenzi holela kutasababisha zoezi hilo kutokuwa na maana kwa kuwa ujenzi holela utakuwa ukiendelea.