Kambi ya madaktari bingwa wa Samia katika Wilaya ya Nsimbo imekuwa mkombozi kwa wagonjwa wenye mahitaji ya matibabu ya kibigwa walioteseka kwa muda mrefu.
Katika kambi hiyo madaktari Bingwa wa magonjwa ya wanawake wamefanikiwa kumfanyia upasuaji mgonjwa aliyesumbuliwa na uvimbe kwenye mayai ya uzazi upande wa kushoto na kulia kwa miaka minne.
Dkt. Emiliana Mvungi Daktari Bigwa wanawake kutoka hospitali ya Rufaa ya Sekouture mkoani Mwanza, amesema kambi hiyo iliyopo katika hosptali ya Wilaya ya Nsimbo wamefanikiwa kuona wagonjwa wenye changamoto mbalimbali na kuhakikisha wanawapatia tiba sahihi bila kuwapa rufaa ambazo zingetumia gharama nyingi.
“Tupo katika hospitali ya wilaya Nsimbo tumeona wagonjwa mbalimbli mmoja wao ni mama wa miaka 24 ambaye alikuwa akisumbuliwa na tumbo kwa miaka mnne tulipokuja hapa tukamfanyia vipimo na kugundulika kuwa ana uvimbe kwenye mayai ya uzazi tukamuelewesha mgonjwa kuhusu ugonjwa wake na matibabu ikawa ni upasuaji”amesema Dkt. Mvungi
Ameeleza, wamefanikiwa kumfanyia upasuaji na kukuta kuwa alikuwa na uvimbe mkubwa pande zote mbili kulia na kushoto na ule uvimbe wa upande wa kulia ulikuwa umekuwa mkubwa na ulikuwa umepasukia tumboni na kuanza kumwaga damu na kusababisha maumivu makali.
“Kwahiyo tumefanikiwa kumfanyia upasuaji na leo tumeona kwamba anaendelea vizuri ameanza kutembea na maumivu yamepungua”ameongeza, Dkt. Mvungi
Vile vile Dkt. Mvungi ameongeza kuwa kupitia ujio huo wa madakatari bigwa wagonjwa wameweza kusaidiwa bila kupata rufaa ya kwenda hospitali kubwa kwakuwa waamesaidiwa wakiwa katika mazingira yao ya karibu na nyumbani.
“Ugonjwa huu hautwezi kusema nini kimesababisha watu wengi wakiwa katika ule umri wa uzazi wanaweza kupata kwasababu yeye ameanza kupata maumivu haya akiwa na umri wa miaka 20 alikuwa akipewa vidonge anatibiwa anakwenda anarudi",
Dkt. Mvungi
“Lakini safari hii maumivu yalikuwa makali sana ambayo hawezi kuyavumilia kwahiyo tulivyo mpima ndiyo tukagundua kuwa na uvimbe kwenye mayai ya uzazi upande wa kulia na kushoto tukamfanyia upasuaji”, amebainishaDkt. Mvungi
Aidha, ameshauri kinamama wanapopata maumivu wasivumilie waende kwenye hospitalini ili kufanyiwa vipimo na kupata huduma sahihi mapema.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Hopitali ya Nsimbo , Dk. Mgaya amesema katika kambi hiyo wamepata madaktari bingwa katika maeneo matano ikiwemo magonjwa ya wanawake,magonjwa ya ndani,upasuaji, tiba ya usingizi na ganzi pamoja na kinywa na meno.
“Ujio wa madaktari hawa bingwa umekuwa ni wa manufaa makubwa sana kwa wananchi wa Nsimbo, kwa maana wagonjwa wengi waliokuwa wanahitaji huduma za kibingwa kwenye maeneo hayo matano na wamefaidika na kupata tiba stahiki na katika mazingira ya karibu na makazi yao.
“Lakini pili watumishi wa wilaya tumejengewa uwezo katika maeneo tofautitofauti hasa tukianza na eneo la upasuaji ambalo tulipata kujifunza mambo mbalimbali ili kesho tunapokutana na kesi kama za namna hiyo inakuwa ni rahisi kuwahudumia walengwa bila kutoa rufaa zisiso za lazima ”ameeleza Dk. Mgaya