Back to top

Madini aina ya Graphite yamegundulika huko wilayani Handeni.

21 December 2018
Share

Madini aina ya Graphite yanayotumika kutengenezea vipuri vya magari na yanayozalisha nishati ambayo pia inatumika kuendeshea magari badala ya kutumia mafuta, yamegundulika huko wilayani Handeni mkoani Tanga.

Kufuatia kugundulika kwa madini hayo tayari wawekezaji wamefika kwenye kijiji kilichogundulika madini hayo cha Kwamsisi kilichopo wilayani Handeni kuanza uwekezaji wa kuchimba madini hayo ambayo ni adimu hapa duniani.

Kufuatia hatua hiyo Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amewataka wawekezaji kufika wilayani hapo hasa kwenye sekta ya madini kwasababu handeni ni moja kati ya wilaya zenye hazina kubwa ya madini.
 
Kufuatia hatua Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Wiliam Makufwe amedai kuwa kupatikana kwa madini hayo kutaiongezea mapato halmashauri yake pamoja na taifa kwa ujumla.