Back to top

MAFUNDI UJENZI MBARONI KWA KUMUUA 'HOUSE GIRL'

02 May 2024
Share

#HABARI: Jeshi la Polisi, Mkoa wa Morogoro limewakamata watu watatu, kwa tuhuma za mauaji ya Monica Paul mwenye umri wa miaka 22, ambaye alikuwa mfanyakazi wa kazi za ndani.
.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema, mmiliki wa nyumba aliyokuwa akifanya kazi binti huyo, ambaye ni mkazi wa mkoani Dar es Salaam, alikuwa akiwatuma watuhumiwa hao, ambao ni mafundi ujenzi, kwenda nyumbani hapo kufanya marekebisho.
.
"Mmiliki wa nyumba ile ambaye ni makazi wa Dar es Salaam...alikuwa akiwatuma mafundi kuja kutengeneza pale nyumbani, kwa hiyo mafundi hao wametumia ule mwanya, kwanza huyu binti ni dhaifu kwa maana alikuwa peke yake,...siku ile ya tukio...wamekuja usiku...wamemgongea mlango, akafungua kwa sababu ni watu anaowafahamu" ameeleza SACP Mkama.
.
Watuhumiwa hao ni Mbaraka Omary (25) fundi ujenzi, mkazi wa Tubuyu, aliyekutwa na televisheni aina ya Hisence inchi 60, redio Sabufa aina ya Boss, spika ndogo za redio hiyo na feni ndogo aina ya Easy Home vilivyoibiwa siku ya tukio na mwingine ni Mussa Mrisho (23) fundi ujenzi, mkazi wa Bigwa ambaye alishirikiana na Mbaraka Omary kutekeleza mauaji hayo pamoja na Rehema Omary (30) mkulima, mkazi wa Mwembesongo, aliyekutwa na simu ndogo ya marehemu aina ya Tecno.