Watu 17 wameripotiwa kufariki dunia, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa, wilayani Hanang Mkoani Manyara kufuatia mafuriko yaliyoambatana na mawe na miti kuingia katika makazi ya watu.
.
Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Bi.Janeth Mayanja, amesema kuwa toka jana usiku zilikuwa zikinyesha mvua za kawaida lakini maji yakawa yameporomoka kutoka Mlima Hanang yakiwa na mawe na miti kuja katika Mji wa Kateshi yakiwa na nguvu.
.
Bi.Mayanja amesema miili ya waliofariki imehifadhiwa katika Hospitali ya Tumaini, huku akibainisha kuwa mawasiliano ya barabara kati ya Singida na Babati yamesimama kwa muda lakini TANROADs na TARURA wanaendelea na juhudi za kuhakikisha mawasiliano hayo yanarejea.