Back to top

MAKAMU WA RAIS WA ZAMANI WA ECUADOR AGOMA KULA

09 April 2024
Share

Makamu wa zamani wa Rais wa Equador, Jorge Glas, ameripotiwa kulazwa katika hospitali ya Jeshi, iliyopo Mjini Guayaquil, baada ya kugoma kula.
.
Makamu huyo wa zamani wa Rais, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 54, alikamatwa siku ya Ijumaa, baada ya vyombo vya usalama vya Equador kuvamia ubalozi wa Mexico, muda mchache tu baada ya kupatiwa hifadhi ya kisiasa kwenye ubalozi huo.
.
Uvamizi huo umesababisha mzozo mkubwa wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo, ambapo Rais wa Mexico, Andrés Manuel López, amemlaumu Rais wa Equador, Daniel Noboa, kwa utawala wa kidikteta.