Back to top

MAMA SAMIA LEGAL AID YAGUSA WANANCHI 415,280

09 April 2024
Share

Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) inayotoa Msaada wa Kisheria bure kwa watu wote, mpaka sasa imefika katika Mikoa 6, Halmashauri 42, Kata 452 na Vijiji/Mitaa 1,348, ambapo imewagusa moja kwa moja Wananchi 415,280 (Wanaume 214,888 wanawake 200,392) miongoni mwao Wafungwa na mahabusu wakiwa 7,166 (Wanaume 6,824 wanawake 342)

Msaada wa Kisheria ni suala linalojumuisha haki na ulinzi wa kisheria kwa watu wote, bila kujali jinsia wala hali ya mtu, ambapo Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) inatoa msaada wa kisheria kwenye migogoro ya ardhi na kuwasaidia wananchi kuelewa vizuri sheria na taratibu zinazohusiana na ardhi.

MSLAC inatoa msaada wa kisheria kwa wanaume/wanawake wanaonyanyaswa na wenza wao, watoto waliokosa haki zao za msingi kutoka kwa wazazi, walezi au jamii inayowazunguka, walemavu ambao wanapitia unyanyasaji, ikiwa ni pamoja na huduma za ushauri nasaha na mafunzo juu ya sheria zinazo walinda.

Aidha MSLAC inatoa Msaada wa kisheria kwa wafungwa na miongozo ya haki za msingi zinazowahusu, inatoa msaada wa kisheria kwa watu walio katika hali ya kukata tamaa, wapweke, na wale ambao wanahisi kwamba sheria imepindishwa dhidi yao.

Pia MSLAC inatoa Msaada wa kisheria kwenye migogoro ya Ndoa, Mirathi, Utawala, Ukatili wa Kijinsia, Matunzo ya Watoto na kutoa elimu ya Masuala yote ya kisheria kwa jamii.

Ili kuhakikisha huduma hii inawafikia wananchi kwa urahisi zaidi, Mashirika 256 yamesajiliwa kwa ajili ya kutoa Msaada wa Kisheria kwa wananchi bila kuwatoza gharama.

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aids, imekuwa msaada mkubwa kwa wanyonge ambao walidhulumia Haki zao.