Back to top

MAMA SAMIA LEGAL AID YAPIGIWA CHAPUO JUMUIYA YA MADOLA

27 February 2025
Share

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, akiwa katika mwendelezo wa kikao cha 58 cha Baraza la Haki za Binadamu Geneva  Nchini, Uswisi amekutana na kufanya mazungumzo yaliyohusu utekelezaji  wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria Nchini Tanzania "Mama Samia Legal Aid " na ujumbe wa Jumuiya ya Madola ukiongozwa na Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Madola Prof.Luis Franceschi jijini Geneva, Uswisi 

Katika mazungumzo hayo,Waziri Ndumbaro alielezea Ujumbe huo ni kwa namna gani Nchi ya Tanzania kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imekua iki tekeleza Kampeni hiyo ambayo imekuwa na Msaada mkubwa kwa Wananchi Watanzania hususani wasio na uwezo wa kumudu gharama za Mawakili  katika utatuzi wa migogoro mbalimbali inayohitaji usaidizi wa Msaada wa Kisheria. 

Waziri Ndumbaro amesema lengo la wasilisho hilo ni kuona ni kwa namna gani Jumuiya hiyo inaweza Kishirikiana na Wizara katika kuifanya Mama Samia Legal Aid kuwa endelevu kwa kutoa Haki kwa Wananchi wenye uhitaji.

Kwa upande wao baadhi ya  Wajumbe wa Baraza la  Haki za Binadamu  wameipongeza Tanzania kwa kuhakikisha inaendelea kusimamia Haki za Binadamu ikiwa ni pamoja kutumia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia . 

Naye, Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Madola Prof. Luis Franceschi baada ya kupokea taarifa ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) ameahidi kusaidia utekelezaji wa Kampeni na kufika duniani kote.