Back to top

"MARUFUKU UKAMATWAJI MIFUGO ISIYOTAMBULIWA"

20 February 2025
Share

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, amepiga marufuku ukamatwaji wa mifugo ambayo haitakuwa imefanyiwa utambuzi na kuwataka watalaam wa sekta ya Mifugo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa zoezi hilo huku akitoa rai kwa wafugaji kutumia fursa iliyotolewa na Serikali kutambua mifugo yao.

Dkt.Kijaji amesema zoezi la Utambuzi wa wanyama sasa litafanyika bila gharama yoyote kutoka kwa wafugaji baada ya Serikali kuamua kugharamia zoezi hilo.

Dkt. Kijaji amesema hayo wakati wa mkutano baina yake na wafugaji uliofanyika Jijini Dodoma, ambao ulilenga kuwahamasisha kuekelea kwenye kampeni ya kitaifa ya chanjo na Utambuzi wa Mifugo.