Back to top

MCHEZAJI WA MTIBWA SUGAR IDDY MOBY AFARIKI

05 March 2023
Share

Mchezaji wa Timu ya Soka ya Mtibwa Sugar, Iddy Moby Mfaume amefariki dunia leo mchana Machi 05, 2023, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, iliyopo Jijini Dodoma, wakati akipatiwa matibabu, ambapo daktari wa Hospitali ya Kampuni ya Mtibwa Sugar, Khalid Sabuni, amebainisha kuwa mchezaji huyo alipata tatizo la kiafya jana, Machi 4, 2023 akiwa mkoani Morogoro wakati akifanya mazoezi binafsi ya barabarani ambapo alifikishwa kwenye hospitali hiyo, kisha hospitali ya Bwagala kwa ajili ya matibabu zaidi lakini ilipofika usiku hali ilikuwa mbaya na hivyo kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Benjamin Mkapa, ambako umauti umemfika.