Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman, amesema Jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja ambaye ni Mfanyabiashara ,mkazi wa Kiyanga, kwa tuhuma za kulawiti kwa nyakati tofauti watoto wa kiume wawili ,wenye umri wa miaka nane, wanafunzi wa darasa la pili Shule ya Msingi Shangani.
Amesema mtuhumiwa amekuwa akitekeleza matukio hayo kwa kuwalaghai watoto hao wakiwa wanatoka shule kuelekea nyumbani na kuwapeleka katika jengo linaloendelea kujengwa, lililopo eneo la maduka makubwa, Manispaa ya Mtwara Mikindani na kuwafanyia vitendo hivyo vya udhalilishaji.
Mtuhumiwa tayari amekamatwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upepelezi kukamilika.