Back to top

MGOGORO WA MALEZI YA MTOTO WATATULIWA

23 February 2025
Share

Timu ya Wataalam wa Msaada wa Kisheria imefanikiwa kutatua mgogoro wa malezi ya mtoto ambaye alishindwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mkotokuyana wilayani Nachingwea. 

Mgogoro huo ulihusisha baba wa mtoto huyo, ambaye awali hakuwa tayari kumhudumia, hali iliyosababisha mtoto kushindwa kuendelea na elimu yake.

Baada ya juhudi za Wataalam hao, baba wa mtoto huyo hatimaye amekubali kuchukua jukumu la kumlea na kuhakikisha mtoto wake anapata elimu anayostahili. 

Hatua hii imeleta faraja kwa familia na jamii ya Kijiji cha Mandai, katika Kata ya Mkotokuyana, kwani itawezesha mtoto huyo kurejea shuleni na kuendelea na masomo yake kama ilivyokusudiwa.

Wakazi wa eneo hilo wamepongeza juhudi za Timu ya Wataalam wa Huduma ya Msaada wa Kisheria kwa kusaidia kupatikana kwa suluhisho la haki kwa mtoto huyo, wakisema kuwa hatua kama hizi ni muhimu katika kuhakikisha watoto wote wanapata fursa sawa ya elimu na malezi bora.