Back to top

MITUNGI 29,000 YATOLEWA KWA BEI NAFUU - SINGIDA

09 March 2025
Share

Katika kilele cha siku ya wanawake dunia Mkoa wa  Singida, imeunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan za kupambana na matumizi ya nishati chafu na kuhamia kwenye nishati safi, kwa kutowa mitungi zaidi ya 29,000 kwa wanawake wa Mkoa wa Singida kwa bei nafuu  ambayo ita zinufaisha kaya 350,000 za mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bi. Halima Dendego, amesema hayo kwenye kilele cha  maadhimisho ya  siku ya  wanawake  kimkoa, ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na kudai kuwa mitungi hiyo itawasaidia wanawake hasa wa vijiji kuboresha afya zao ambazo zilikuwa zikiathirika na moshi wa kuni.

Kwaupande wao baadhi ya wanawake walio patiwa mitungi hiyo  wamesema matumizi ya gesi yatawasaidi kuondokana na magonjwa yatokananyo na moshi, huku  Afisa wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji  Mkoa wa Singida, Rahma Abdarabi, ametoa mafunzi ya kwa namna gani moto unaosababishwa na gesi unadhibitiwa ilikujikinga na kutumia mitungi kwa uagalifu  kwa kuhakikisha mtungi unazimwa kila unapo maliza matumizi

Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dk. Fatuma Mganga, amesema  mkoa umefanya shughuli za matendo ya uhuruma kwa kutowa misaada mbalimbali kwa wenye mahitaji na wanawake walio lazwa kwenye hospita mbalimbali.

Maadhimisho yameenda pamoja na maandamano  maonyesho mbalimbali ikiwemo shughili zinazo fanywa na wanawake  za  ulinzi , kuendesha mitambo   mikubwa ya ujenzi na jinsi ya kuzima moto.