Back to top

Mkandarasi aagizwa kukamilisha miradi ya barabara kabla ya April 2019

26 August 2018
Share

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti ameagiza kampuni ya ukandarasi wa NCL International inayofanya kazi ya ujenzi wa miradi minne ya barabara zilizoko katika manispaa ya Bukoba zenye urefu wa zaidi ya kilomita 5 zinazojengwa kwa kiwango cha Lami nzito kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7, fedha iliyotolewa na benki ya dunia kupitia programu yake ya uimarishaji wa miji (ULGSP), kukamilisha miradi hiyo kabla ya mwezi April mwaka ujao.

Brigedia Jenerali Gaguti aliyekagua kazi ya utekelezaji wa miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuzindua ujenzi wake kwa kuweka jiwe la msingi katika eneo la mradi wa barabara unaofanyika katika kata ya Nshambya amesema miradi hiyo ikikamilika mapema itakuwa chachu ya maendeleo ya mji wa Bukoba na itawawezesha wananchi katika mji huo kuondokana na usumbufu wanaoupata kwa sasa wa kutumia barabara za muda zilizojengwa na mkandarasi huyo zinazopitika kwa shida hasa wakati wa kipindi cha mvua kauli ya kukamilisha miradi hiyo kwa wakati imeungwa mkono na mkurugenzi wa kampuni ya ukandarasi, Mauhuza Mumangi aliyeahidi kukamilisha miradi hiyo kwa muda uliopangwa.

kwa upande wake,mratibu wa programu ya  (ULGSP) katika manispaa ya Bukoba, Mhandisi Andondile Mwakitalu akizungumza amesema mradi minne inayotekelezwa katika manispaa hiyo kwa sasa iko katika hatua za awali na  ameyataja maeneo mengine ya miradi ya barabara kuwa ni pamoja na ufukwe wa ziwa Victoria, Nyangoye na Binsaid, naye Joseph Nyirenda mhandisi mshauri wa miradi hiyo amesema changamoto za mradi kuwa ni pamoja na miundombinu iliyoko kwenye barabara ambayo ni pamoja na mabomba ya maji, miamba na nguzo za umeme.