Back to top

Mkurugenzi wa jiji la Mwanza aingia 18 za Majaliwa, apewa siku 7.

17 December 2020
Share

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amempa siku 7 Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kujieleza kwa nini amenunua gari ya fahari aina ya VXR - V8 kwa gharama ya Shilingi Milioni 270.

Wakurugenzi wengine walioagizwa na Waziri Mkuu kujieleza kwa matumizi mabaya ya fedha za umma ni pamoja na wa Chato, Msalala na Kahama.

Waziri Mkuu Majaliwa pia amehoji gharama za mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi na malori eneo la Nyamhongolo Manispaa ya Ilemela, baada ya kuonekana za juu zaidi, wakati kulikuwa na mkandarasi aliyepaswa kupewa zabuni ya ujenzi wa stendi hiyo kwa bei ndogo.

Pia Waziri Mkuu amefuta likizo zote kwa watumishi wa Idara ya Elimu, Wahandisi wa Majengo, Maafisa Ununuzi pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya ili kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ya sekondari.