Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mary Makondo, amesema Wizara hiyo chini ya Kampeni ya Mama Samia Legal Aid, imeendelea kuwapokea Wananchi, kuwafikia kwa karibu na kuwasogezea huduma za msaada wa kisheria katika masuala ya Elimu, utatuzi wa migogoro, mahitaji na taratibu za kisheria ambazo wananchi wanapaswa kuzielewa.
Bi.Mary Makondo ametoa rai kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya msaada wa kisheria bure hasa kwenye eneo la mirathi na Wosia ambalo limekuwa na migogoro mingi inayopokelewa kwenye kituo Jumuishi cha Temeke kuanzia Mahakama ya chini hadi Mahakama ya juu Kabisa ya Rufani ambapo maombi ya mirathi yasiyopungua 600 yamewasilishwa.
Ameeleza hayo alipo tembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria lililopo kwenye maonesho ya Sabasaba Jijini Da- es Salaam, Katibu Mkuu huyo amesema mwitikio umekuwa ni mkubwa, Wananchi wamejitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata misaada mbalimbali ya kisheria inayotolewa bure kupitia Mama Samia Legal Aid Campaign.
"Tunamshukuru Rais wetu wa awamu ya sita Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye kibajeti ametuwezesha kama Wizara kupitia Waziri mwenye dhamana Mhe. Pindi Chana kuweza kugharamia huduma za vyeti vya kuzaliwa bure kwa Watoto wote wenye umri wa chini ya miaka mitano na Watoto wenye umri zaidi ya huo wanalipia ada kidogo sana" -Bi.Mary Makondo - Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
Ametoa rai kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya msaada wa kisheria bure hasa kwenye eneo la mirathi na Wosia ambalo limekuwa na migogoro mingi inayopokelewa kwenye kituo Jumuishi cha Temeke kuanzia Mahakama ya chini hadi Mahakama ya juu Kabisa ya Rufani ambapo maombi ya mirathi yasiyopungua 600 yamewasilishwa.
Amesema eneo jingine lenye shida ni talaka na ndoa na Wanawake wengi wamepitia ukatili wa kijinsia, masuala ya kutelekeza familia na wakati mwingine pamoja na kwenda Wizara ya maendeleo ya jamii bado hakuna mwitikio hivyo Serikali imelichukua hilo kwa kushirikiana na wadau wote ili wale wote wanaokutana na kadhia za aina hiyo waweze kupata msaada.