Mkuu wa mkoa wa Kagera brigedia jenerali Marco Elisha Gaguti amemuagiza kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo kuwasaka na kuwatia mbaroni wafanyabiashara wanaojihusisha na vitendo vya kuwalaghai wakulima wa zao la kahawa wa wilaya za Kyelwa na Karagwe wasiuze kahawa zao kwenye vyama vya msingi vilivyoko katika wilaya hizo badala yake waifiche majumbani mwao ili wauze kahawa yao kwa walanguzi toka nchi jirani kwa bei kubwa pale msimu wa ununuzi wa kahawa wa mwaka 2019/2020 utakapomalizika.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa agizo hilo baada ya kukagua viwanda vya kukoboa kahawa cha Kharim Amri na kufanya mazungumzo viongozi wa vyama vya msingi vilivyoko katika wilaya hizo, amesema serikali itawachukulia hatua wale wote watajihusisha na vitendo vya magendo ya kahawa bila kuangalia sura zao, nyazifa zao na nafasi zao walizonazo ndani ya jamii.
Aidha, amesema katika kupambana na magendo ya kahawa mkoa huo kuanzia mwezi wa 8 unatarajia kuwahamisha wananchi wachangamkie fursa ya mfumo wa mfuko wa mazao ghalani.
Nao baadhi ya viongozi wa vyama msingi wakizungumza wameushauri uongozi wa chama cha maendeleo ya wilaya ya Karagwe KDCU uweke mfumo mzuri wa malipo ya wakulima ili uondoe malalamiko yanayotolewa na wakulima hao.