Mwanafunzi wa darasa la tano amefariki na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya mabweni matatu ya shule ya St.Joseph Rutabo mkoani Kagera kuungua moto.
Kwa Mujibu wa Mwandishi wetu Audax Mutiganzi aliyefika katika eneo la tukio anaeleza kuwa hii ni mara ya pili kuungua kwa mabweni hayo ambapo miezi miwili nyuma liliungua bweni moja na sasa mabweni matatu, hali ambayo imesababisha vifaa vya wanafunzi kuteketea moto.
Moto huo umefanikiwa kuzimwa na wananchi kutokana na kutokuwepo kwa gari la kuzimia moto katika eneo hilo, kwani Mpaka sasa chanzo cha moto bado hakijajulikana mara moja mamlaka husika zinaendelea kufuatilia.
Kujua zaidi Nimekuwekea video hapa.