Naibu rais mteule wa Kenya, Kindiki Kithure, ataapishwa hapo kesho katika jumba la mikutano la KICC.
Ikumbukwe kuwa leo Mahakama Kuu jijini Nairobi ilifutilia mbali agizo la Mahakama ya Kuu ya Kerugoya, Kaunti ya Kirinyaga kuzuia kuapishwa kwa Prof. Kithure Kindiki kama Naibu Rais.
Jopo la majaji watatu wakiongozwa na Erick Ogolla, lilisema limechukua uamuzi huo kwa kuzingatia kwamba Ofisi ya Naibu Rais haiwezi kuendelea kusalia bila kuwa na mtu.
Uamuzi huu sasa unaruhusu kuapishwa kwa Kithure Kindiki kama Naibu Rais wa Tatu wa Kenya.
Hata hivyo, Jaji Ogolla amesema Gachagua anaweza kuukatia rufaa uamuzi huo.
Katika hatua nyingine Musalia Mudavadi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje nchin Kenya ameteuliwa kuwa Kaimu Waziri wa Usalama wa Kitaifa.