Back to top

NAIBU WAZIRI PINDA AONYA MAAFISA ARDHI WANAOKIUKA MAADILI

20 September 2024
Share

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Geophrey Pinda, amesema kuwa hakuna afisa Ardhi atakayehamishwa eneo la kazi, endapo atakiuka maadili ya utendaji wa taaluma yake.

Amebainisha hayo katika mkutano wa pamoja wa wananchi na watumishi wa Ardhi, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Ametoa maelekezo kwa ofisi za Wasajili wa Hati nchini, kuharakakisha mchakato wa utoaji hatimiliki za Ardhi, ili wananchi waweze kunufaika nazo, ikiwa pamoja na kuaminiwa kupata mikopo katika taasisi za kifedha.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Ardhi, amewaonya Maafisa Ardhi wanaojiuhusisha na ugawaji kiwanja  kimoja mara mbili na kusisitiza kuwa Wizara yake, itachukua hatua kali za kinidhamu dhidi ya mtumishi yeyote atakayekiuka maadili ya utumishi wa umma kwa taaluma yake.

Naibu Waziri Mhe.Pinda amehitimisha ziara yake mkoani Kilimanjaro jana ambapo mbali mambo mengine alisikiliza na kutatua changamoto za ardhi kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na kufanya vikao kazi na watumishi wa Ardhi mkoani humo.