Back to top

NYANGUMI 'JASUSI WA URUSI' AFARIKI GHAFLA.

02 September 2024
Share

Nyangumi anayetajwa kuwa ni jasusi wa Urusi, aliyejulikana kama Hvaldimir, amekutwa amekufa na mwili wale kukutwa ukielea kwenye Ghuba ya Risavika Kusini mwa Norway, siku ya Jumamosi, na watu wawili ambao ni baba na mwanawe waliokuwa wakivua samaki.

Mwanabiolojia wa baharini Sebastian Strand, ambaye amemchunguza nyangumi kwa miaka mitatu iliyopita, alisema haijulikani ni nini kimemuua Hvladimir, na kuongeza kuwa hakuna majeraha makubwa ya nje yalionekana.

Regina Crosby Haug kutoka shirika la One Whale, ambalo lilifanya kampeni ya kumlinda Hvaldimir, alinukuliwa akisema "nyangumi mchanga mwenye afya njema asiye na dalili za ugonjwa".

“Hvaldimir hakuwa nyangumi wa beluga tu; alikuwa mwanga wa matumaini, ishara ya uhusiano, na ukumbusho wa uhusiano wa kina kati ya wanadamu na ulimwengu wa asili," Marine Mind, shirika lisilo la faida ambalo lilikuwa likifuatilia mienendo yake, lilisema kwenye mitandao ya kijamii.

Hvaldimir, ni mchanganyiko wa neno lenye asili ya Norway la nyangumi, "hval", na jina la kwanza la Rais wa Urusi Vladimir Putin, na nyangumi huyo alionekana kwa mara ya kwanza kwenye pwani ya kaskazini ya Norway mnamo 2019.