Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Geophrey Pinda, amekitaka Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) kufanya maboresho kwenye sehemu yake ya uchapishaji ili kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia.
Mhe.Pinda ametoa kauli hiyo Chuo cha Ardhi Tabora ikiwa ni jihudi zake za kuhakikisha chuo cha ARITA kinafanya kazi kwa ifanisi na kutoa huduma bora za uchapishaji.
Amesema, uboreshaji sehemu ya uchapishaji ndani ya chuo hicho kutakiwezesha chuo kupata kazi nyingi za uchapishaji na hivyo kukiingiza pesa.
Naibu Waziri ameutaka uongozi wa chuo hicho cha Ardhi Tabora kuandika gharama za vifaa vya kisasa ili aoene namna ya kukisaidia kupata vifaa vya kisasa vitakavyokiwezesha chuo kuingia kwenye ushindani wa kibiashara.
Aidha, ameutaka uongozi wa chuo cha ARITA kwenda kuiifunza kwa taasisi nyingine kama vile Taasisi ya Uchapishaji ya Serikali (Government Printers) ili kuona namna bora ya kuimarisha sehemu hiyo ili kiweze kufanya vizuri kwenye utendaji kazi wake.
Awali Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora Juma Mkuki amemueleza Naibu Waziri Mhe. Pinda kuwa, chuo chake kinaendesha mafunzo pamoja na shughuli za uchapishaji kwa kushirikiana na wizara pamoja na wadau wegine ambapo chuo hicho kinazalisha machapisho mbalimbali kwa idara za serikali, taasisi na mashirika mbalimbali kama sehemu ya kujiongezea kipato.
Kwa mujibu wa Mkuki, kuanzia mwaka 2019/2020 hadi sasa chuo kinazlisha machapisho ya nyaraka mbalimbali zinazotumiwa na wizara ya ardhi kwa ajili ya kumilikisha ardhi na usajili kwa ujumla.
Kaimu Mkuu huyo wa chuo cha Ardhi Tabora, amesema, sehemu ya uchapishaji inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maabara kwa ajili ya uchapishaji,
Hata hivyo, ameeleza kuwa, pamoja na chuo kujitahidi kutafuta mitambo na vifaa vya uchapishaji lakini jengo linalotumika ni dogo hivyo chuo hicho cha ARITA kiko kwenye hatua za kuhakikisha jengo hilo linajengwa kwa kushirkiana na wadau nje ya chuo.