Back to top

POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WAPONGEZWA

11 October 2024
Share

Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa kipolisi Kinondoni (RTO), Solomon Mwangamilo, ameushukuru Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kutambua utendaji mzuri wa jeshi hususan kikosi cha usalama barabarani.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wa hafla fupi ya kumpongeza askari wa usalama barabarani Mkoa wa Kinodnoni, Koplo Ashraf Shabani, wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwenye ofisi za PSSSF Kanda ya Kinodnoni, Dar Es Salaam.


“Nyie mnaweza kuona ni jambo la kawaida, kwetu sisi kama jeshi la polisi sio la kawaida, watu wengi wamekuwa wakitanguliza lawama, lakini nyie mmeonyesha wengine wanatambua kazi nzuri tunayofanya tunawashukuru sana.” Alisema RTO Mwanagamilo.


Naye Meneja wa PSSSF Kanda ya Kinodnoni, Bw. Hajji Khamisi, amesema kwaniaba ya wafanyakazi wa PSSSF hususan ofisi ya Kanda ya Kinodnoni, wanalishukuru jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao katika kuongoza magari.


“Sisi tuna ofisi hapa Kinodnoni, tuna ofisi Temeke, lakini pia tuna ofisi makao makuu ndogo Dar Es Salaam pale Posta, wafanyakazi wetu wanategemea sana utendaji mzuri wa askari wa usalama barabarani kuwahi makazini, na sisi tumeona kwenye hili mnajitahidi na mnastahili pongezi.” Amesema Khamisi.