Back to top

POLISI WATAKIWA KUDHIBITI UHALIFU KWA VITENDO

15 March 2025
Share

Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dkt. Lazaro Mambosasa, amewataka wanafunzi wa Kozi ya Uafisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kuzingatia kwa vitendo mbinu na maarifa wanayopewa katika kudhibiti vitendo vya kihalifu.

Dkt. Mambosasa ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanafunzi hao chuoni hapo, ikiwa ni utaratibu wa kawaida wa kuzungumza na wanafunzi hao kwa lengo la kufanya tathimini ya mafanikio na changamoto mbalimbali ikiwemo za kitaaluma ili kuzipatia ufumbuzi.

Amesema Jeshi la Polisi limeendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya kitaaluma na kufundishia itakayomsaidia Afisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi pindi atakapohitimu kwenda kutekeleza majukumu ya kazi za Polisi kwa weledi, nidhamu na uadilifu na kuhakikisha anatenda haki kwa wateja atakaowahudumia.